TAMTHILIA ya ‘Be
Careful with my Heart itaendelea leo usiku kwa kumuonyesha Rafi na Charlie, na
baada ya kuvishana pete wanaonekana kutokuendelea kuishi katika nyumba ya Lim.
Lakini wakiwa
wanajiandaa kuondoka katika nyumba hiyo, Maya, na watu wengine katika nyumba
hiyo wanapanga kumfanyia sherehe ya kumuaga Rafi na Charlie.
Katika
sherehe hiyo, wakapanga wawe wawili wawili ili kuvutia tafrija hiyo lakini kila
mmoja anapata wa kucheza naye isipokuwa Maya anajikuta akiwa peke yake.
Maya
baada ya kujiona yupo peke yake anasema hajali kuimba akiwa peke yake lakini
licha ya hivyo wimbo wa Maya unatakiwa uimbwe na watu wawili kutokana na sauti
ya kike na ya kiume.
Anaanza
kuimba kwa hisia kubwa, inawagusa watu wote akiwemo Richard. Lakini licha ya
yote anapatwa na mshangao, baada ya kusikia sauti ya kiume ikiimba tena ni ya
Richard, lakini sauti hiyo ilikuwa inaimba kwa kutokwenda na biti jambo
lililozua kicheko zaidi.
Wakiwa
wanaelekea uwanja wa ndege, Rafi anampigia Richard anamtaka amwahidi kama
atampigia simu kama atampata msichana atakayempenda tena kama ilivyokuwa kwa
marehemu mke wake.
Richard
anakubaliana na hilo huku akitabasam mwenyewe. Baada ya muda, Kutengana kwa
Cristina Rose (kute) na mtoto wake kunazua matatizo makubwa tofauti na
alivyokuwa akifikiria awali.
Hali
hiyo inamfanya azungumze na viongozi wake huku akiwaeleza kwamba anapenda
kufanyakazi katika meli aamini kama mtoto wake anaweza kukua bila kuwa karibu
yake.
Maya
anapanga tarehe ya kukutana na Simon lakini anapata simu kutoka kwa Richard
akimuomba amsaidie kumtafutia Abby rafiki wa kucheza naye lakini Maya
anapozungumza na Abby anamweleza kwamba ingawa hakuna michezo ya kuangushana
lakini urafiki wao unaendelea kama kawaida.
Lakini
licha ya hayo anamwahidi Abby kwamba atamtafutia rafiki mara tu atakaporejea.
Mara baada ya Maya kurudi nyumbani, Richard anajifanya kama hajali huku
akionekana mwenye hasira.
Maya
anahofia hali ya upole wa bosi wake, anamuomba msamaha huku akimweleza kwamba
hakutaka amsumbue kwa kuwa anakazi lakini ukweli ni kwamba aanacheza ‘gemu’ la
karata katika kompyuta yake mpakato.
Maya
anamweleza Miss Fe kuhusu ukimya wa Richard. Miss Fe anamwakikishi kwamba Richard
hawezi kuigiza vile kama amwofii Maya na maisha yake ya baadae. Maya anaonekana
kufurahia jambo hilo kusikia Richard anamjali katika hilo.
Siku
ya pili asubuhi, Richard anasikia mazungumzo ya Maya na Simon. Simon anataka
kuwachukua Cristina Rose na Maya hadi stendi. Maya anakubali lakini Richard anajitolea
kuwachukua Maya na Cristina Rose hadi stendi huku akionekana mnyenyekevu kwao.