Tuesday, November 6, 2012

IN THE MAKING OF MGUU KWA MGUU FILM

Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa wakati wa kuigiza filamu ya Mguu kwa Mguu inayotarajiwa kutoka mwanzoni mwa Desemba mwaka huu, katika filamu hiyo utakutaa na wasanii wenye majina akiwemo Salma Salimini (Sandra) na wengine wengi. Si ya kukosa.
 Msanii Eva katikati akiwa na mtoto wake aliyepotezana naye miaka mingi hapa baada ya kuonana naye kulia ni mama yake mzazi lakinii kwenye filamu ya mguu kwa mguu inayotarajiwa kuingia sokoni mwanzoni mwa Desemba.
 Baba na mama Eva wakitafakari jambo kuhusu mtoto wao hapa wanajianda kushuti filamu ya Mguu kwa Mguu
 France akiwa amelala na Vanessa baada ya kukutana naye mtaani hivyo alikwenda kumjulia hali kutokana na kuumia mguu wakajikuta wakiingia katika maoenzi mazito yote hayo ndani ya Filamu ya Mguu kwa Mguu
 Baada ya kuchoka walilala kwa safari ndefu ya kutafuta location katika kijiji cha Homboza kilichopo mkoani Pwani
Usingizi uliendelea hapa hapakuwa na mazungumzo kimya kilitawala yote ni ndani ya 'Mguu kwa Mguu'