Tuesday, July 1, 2014

BE CAREFUL WITH MY HEART - RICHARD WIVU TUPU KWA MAYA





TAMTHILIA ya ‘Be Careful with my Heart itaendelea leo usiku kwa kumuonyesha Rafi na Charlie, na baada ya kuvishana pete wanaonekana kutokuendelea kuishi katika nyumba ya Lim.
     Lakini wakiwa wanajiandaa kuondoka katika nyumba hiyo, Maya, na watu wengine katika nyumba hiyo wanapanga kumfanyia sherehe ya kumuaga Rafi na Charlie.
     Katika sherehe hiyo, wakapanga wawe wawili wawili ili kuvutia tafrija hiyo lakini kila mmoja anapata wa kucheza naye isipokuwa Maya anajikuta akiwa peke yake.
     Maya baada ya kujiona yupo peke yake anasema hajali kuimba akiwa peke yake lakini licha ya hivyo wimbo wa Maya unatakiwa uimbwe na watu wawili kutokana na sauti ya kike na ya kiume.
        Anaanza kuimba kwa hisia kubwa, inawagusa watu wote akiwemo Richard. Lakini licha ya yote anapatwa na mshangao, baada ya kusikia sauti ya kiume ikiimba tena ni ya Richard, lakini sauti hiyo ilikuwa inaimba kwa kutokwenda na biti jambo lililozua kicheko zaidi.
       Wakiwa wanaelekea uwanja wa ndege, Rafi anampigia Richard anamtaka amwahidi kama atampigia simu kama atampata msichana atakayempenda tena kama ilivyokuwa kwa marehemu mke wake.
      Richard anakubaliana na hilo huku akitabasam mwenyewe. Baada ya muda, Kutengana kwa Cristina Rose (kute) na mtoto wake kunazua matatizo makubwa tofauti na alivyokuwa akifikiria awali.
      Hali hiyo inamfanya azungumze na viongozi wake huku akiwaeleza kwamba anapenda kufanyakazi katika meli aamini kama mtoto wake anaweza kukua bila kuwa karibu yake.
       Maya anapanga tarehe ya kukutana na Simon lakini anapata simu kutoka kwa Richard akimuomba amsaidie kumtafutia Abby rafiki wa kucheza naye lakini Maya anapozungumza na Abby anamweleza kwamba ingawa hakuna michezo ya kuangushana lakini urafiki wao unaendelea kama kawaida.
       Lakini licha ya hayo anamwahidi Abby kwamba atamtafutia rafiki mara tu atakaporejea. Mara baada ya Maya kurudi nyumbani, Richard anajifanya kama hajali huku akionekana mwenye hasira.
     Maya anahofia hali ya upole wa bosi wake, anamuomba msamaha huku akimweleza kwamba hakutaka amsumbue kwa kuwa anakazi lakini ukweli ni kwamba aanacheza ‘gemu’ la karata katika kompyuta yake mpakato.
     Maya anamweleza Miss Fe kuhusu ukimya wa Richard. Miss Fe anamwakikishi kwamba Richard hawezi kuigiza vile kama amwofii Maya na maisha yake ya baadae. Maya anaonekana kufurahia jambo hilo kusikia Richard anamjali katika hilo.
     Siku ya pili asubuhi, Richard anasikia mazungumzo ya Maya na Simon. Simon anataka kuwachukua Cristina Rose na Maya hadi stendi. Maya anakubali lakini Richard anajitolea kuwachukua Maya na Cristina Rose hadi stendi huku akionekana mnyenyekevu kwao.


ARGENTINA NA UBELGIJI ZAFUZU ATUA YA MTOANO KOMBE LA DUNIA



USWISI ikiongozwa na Xherdan Shaqiri katika ushambuliaji imeshindwa kutamba mbele ya Argentina iliyoongozwa na Lionel Mess,ambayo imeifunga Uswisi kwa goli 1.
Uswisi ilikuwa na ukuta mgumu na mpira ulioeleweka lakini safu ya umaliiaji ilikuwa butu baada ya kukosa magoli mengi. Hata hivyo kipa alikuwa na uwezo mkubwa wa kuokoa michomo kutoka kwa washambuliaji wa Argentina akiwemo Maria na Messi.


        Wakati huo huo,  Marekani nayo imetupwa nje ya mashindano hayo na Ubelgiji, baada ya kufungwa magoli 2-1. Marekani walikuwa na bahati lakini hawakuitumia vizuri kwani walipata nafasi nyigi za wazi za kufunga lakini walishindwa kufanya hivyo.      
          Hatua inayofuatwa itaendelea Ijumaa baada ya kuwa na mapumziko ya siku mbili kwa timu zilizofuzu atua inayofuata kujipanga kwa mechi zao.


NIGERIA, ALGERIA NJE




BRASILIA, BRAZIL


TIMU ya soka ya Taifa la Nigeria imeaga fainali za Kombe la Dunia 2014, baada ya kufungwa mabao 2-0 na Ufaransa kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo inayoendelea nchini Brazil na Ufaransa imetinga hatua ya robo fainali.
    Kichwa la Paul Pogba dakika ya 78 ilififisha matumaini ya Nigeria kupata ushindi na kama haitoshi, Joseph Yobo alijifunga dakika ya pili ya muda wa dakika tano za nyongeza, na hivyo kuihakikishia Ufaransa tiketi ya robo fainali.
Kwa muda mrefu wa mchezo huo, kipa wa Nigeria, Vincent Enyeama – ambaye anakipiga katika klabu ya Lille ya Ufaransa, alifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya hatari ya Ufaransa, lakini kwa bahati mbaya alifanya kosa lililomzawadia bao Pogba, mchezaji wa zamani wa Manchester United ambaye kwa sasa anakipiga Juventus.
           Hadi dakika ya 77, Enyeama alikuwa shujaa wa Nigeria, akiwa ameokoa bao lililotokana na shuti la Mathieu Valbuena aliyetengewa mpira na Pogba.
       Nayo Algeria ilijikuta katika wakati mgumu wa kutolewa katika mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani.