Monday, May 11, 2015

Chris Brown agombea mtoto na raia wa Brazil





NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, ameonekana kuendelea kumgombea mtoto anayedaiwa kuwa na mgogoro wa baba sahihi kati yake na raia wa Brazil, King Ba.
Baada ya hali hiyo Chris Brown ameonekana akifanya juhudi za kupata cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo ili atambulike kuwa ndiye baba mzazi na juhudi hizo zinafanywa na mwanasheria wake.
Juhudi hizo alizianza baada ya kusherehekea miaka 26 ya kuzaliwa kwake akiwa na mastaa mbalimbali akiwemo bondia Floyd Mayweather.
Sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Drai’s uliopo Las Vegas nchini humo ikiwa na mvuto huku mtoto huyo aliye kwenye mgogoro akiwa kivutio kikubwa baada ya kuonyeshwa katika Runinga huku ukipigiwa wimbo wa Royal.

Bob junior, Diamond kurudi pamoja





BAADA ya kushangaza wengi alipohudhuria katika sherehe ya Zari All White Party iliyoandaliwa na msanii Abdul Nasib ‘Diamond’ anayedaiwa kutoelewana naye, prodyuza Raheem Rummy ‘Bob junior’ ameendelea kushangaza wengi kwa madai kwamba wapo mbioni kurekodi wimbo wa pamoja na msanii huyo.
Prodyuza huyo aliweka wazi mipango yake hiyo huku akidai tayari ameishanunua baadhi ya vifaa vipya kwa ajili ya kuimarisha studio yake iwe katika ubora wa kimataifa kama studio nyingine zinazoongoza kwa ubora duniani.
“Hiyo ni zaidi ya ‘surprise’, kwa ubora wa vyombo vyangu ninaimani ‘beat’ itakayotoka hapo itakuwa kwenye kiwango cha hali ya juu na kazi yetu itakuwa nzuri sana,” alimaliza.
Source Mtanzania