Montevideo,
Uruguay
MCHEZAJI, Luis Suarez ameomba radhi kwa
beki wa Italia, Giorgio Chiellini, baada ya kumng’ata katika fainali za Kombe
la Dunia siku waliyocheza na timu hiyo kuitupa nje Italia katika fainali hizo zinazoendelea nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay, amefungiwa
miezi minne na mechi tisa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), baada ya
tukio hilo.
Awali mchezaji huyo alikataa kata kata kumng'ata beki huyo lakini jana amekubali jambo hilo ambalo hata hivyo baadhi ya watu wanadai amelazimishwa kufanya hivyo.
Katika maelezo yake aliyoyatoa katika
mtandao wa Twitter, Suarez, aliandika: “Baada ya kuwa nyumbani siku kadhaa na
familia yangu, nilikuwa na nafasi ya kukumbuka yaliyotokea katika mechi yetu na
Uruguay. Najuta kwa kile nilichofanya.”
“Naomba msamaha kwa Giorgio Chiellini na
wapenda soka wote. Naapa kwa jamii kuwa sitarudia tena tukio kama hilo.”
Lakini kabla ya kuomba msamaha, Rais wa Uruguay,
Jose Mujica, aliitukana FIFA kutokana na kifungo hicho cha miezi minne na mechi
tisa cha Suarez.
No comments:
Post a Comment
Comment