TIMU ya soka ya Taifa la Nigeria imeaga fainali za Kombe la Dunia 2014, baada ya kufungwa
mabao 2-0 na Ufaransa kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano hiyo
inayoendelea nchini Brazil na Ufaransa imetinga hatua ya robo fainali.
Kichwa la Paul Pogba dakika ya 78 ilififisha matumaini ya Nigeria kupata ushindi na kama haitoshi, Joseph Yobo alijifunga dakika ya pili ya
muda wa dakika tano za nyongeza, na hivyo kuihakikishia Ufaransa tiketi ya robo
fainali.
Kwa muda mrefu wa mchezo huo, kipa wa Nigeria, Vincent
Enyeama – ambaye anakipiga katika klabu ya Lille ya Ufaransa, alifanya kazi ya
ziada kuokoa michomo ya hatari ya Ufaransa, lakini kwa bahati mbaya alifanya
kosa lililomzawadia bao Pogba, mchezaji wa zamani wa Manchester United ambaye
kwa sasa anakipiga Juventus.
Hadi dakika ya 77, Enyeama alikuwa shujaa wa Nigeria, akiwa
ameokoa bao lililotokana na shuti la Mathieu Valbuena aliyetengewa mpira na Pogba.
Nayo Algeria ilijikuta katika wakati mgumu wa kutolewa katika mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani.
No comments:
Post a Comment
Comment