Amante anapigwa risasi, Gary anaziona fedha zilizofichwa
Msomaji wa safu hii nakukaribisha katika muendelezo wa simulizi hii ya ‘Mara Clara’ wiki hii tuanze kwa kumuangalia Gary akimkaribisha Alvira kwake, Alvira analazimika kukubali ili kufanikisha mpango wake kuhusu mtekaji wa watoto na fedha zake alizozipeleka kwa watekaji.
Gary anamchukua Alvira hadi kwa Lupe ambapo anatangaza kuwa wataoana siku za karibuni. Muda unapokwenda, Alvira anaingiwa na hofu kutokana na mpango huo.
Amanthe anapokea taarifa kutoka kwa mpelelezi wake binafsi kuwa waende sehemu ambayo Gary atafika kwa ajili ya makabidhiano ya dawa za kulevya.
Lakini Amante anapigwa risasi na Gary David, anakimbizwa hospitalini, Alvira anapopata taarifa anashindwa kwenda anamuuliza Yaya Vonnel sehemu alipopelekwa lakini anajibiwa kuwa haijui. Anajaribu kupiga simu Amante lakini haipatikani wakati huo Gary anarudi nyumbani kwake akiwa na furaha ya kumpiga risasi Amante, anamweleza mama yake kuwa mipango yake yote imefanikiwa.

Anamweleza kuwa mpango wake mpya ni kufunga ndoa na Alvira. Akiwa amelewa Gary anakwenda kwa Alvira anamweleza kuwa wapo huru wanatakiwa kujipongeza kwa hilo lakini licha ya hayo Alvira anafanikiwa kwenda hospitali lakini anakwenda huku akiwa na hofu kubwa juu ya hali ya Amante. W
akati huo Gary naye anamfuatilia kibaya zaidi anamuona akilia mbele ya Amante anagundua kuwa anamdanganya kwa kuwa bado anampenda Amante.
Back home, Susan David anampigia Alvira na kumweleza kuwa wanatarajia kurudi, Alvira anamtaka Susan kuwa katika safari hiyo kwa kuwa Amante ameshapigwa risasi na Gary.
Gary akiwa mwenye hasira anarudi kwake anamweleza Clara kuwa ameshagundua kuwa Alvira hampendi kweli bali anamuigizia, Clara anamwambia kuwa Alvira anampenda Amante siyo yeye. Hayo yakiendelea kabla Gary hajampigia Alvira, Alvira anampigia Susan, ili kujua kama wameshafika.
Suzan anampa simu Mara ili azungumze na mama yake hivyo kwa mara ya kwanza Mara anazungumza na mama yake anamuuliza kuhusiana na hali ya baba yake huku Alvira anamsisistizia kuwa makini zaidi kwa kuwa Gary ndiye aliyempiga risasi baba yake.
Lupe anajaribu kumweleza Clara amsaidie kuchimba sehemu alipoficha fedha ili ziwe ushahidi katika kesi ya Mara lakini Clara hamwelewi zaidia anahisi kuwa anampigia kelele. Gary anaporudi anamuuliza Clara kinachoendelea Clara anamweleza Gary kuwa alikuwa akipiga kelele huku akionyesha nje ya nyumba yao huku akijaribu kunieleza kitu lakini hakumuelewa.
Gary anakwenda nje ya nyumba yake na kuanza kutafuta hatimaye anakuta fedha zilizofichwa chini ya udongo, fedha ambazo alizipata baada ya kumteka Mara. Gary anapata furaha tena na kumshukuru mama yake kwa kuficha fedha hizo nay eye kuwa wa kwanza kuzigundua.
Mara, Susan na Derek wamerudi hadi Manila, Mara na Suzan wanafika nyumbani kwa Alvira huku Gary akiendelea kumtishia Alvira kwa bundunki akimlazimisha kwenda naye anakotaka yeye.
Wakati hayo yakiendelea hali ya Amanthe inatengamaawakati huo, Gary anampigia Clara ili kuiomba familia ya Del Valles ifute kesi dhidi ya baba yake lakini familia hiyo inakataa kuifuta.
Gary anarudi nyumbani kwake akiwa na hasira lakini hamkuti mama yake, Mara na Susan wamemchukua Lupe kwa msaada wa CG. Lakini wakiwa katika harakati za kutaka kuondoka eneo hilo Lupe anawaeleza kuwa anataka kwenda nao nyumbani kwake kwa kuwa kuna jambo anataka kuwaeleza. Wakati Lupe akisema hayo Suzan na Mara wanamshangaa kumuona akiweza kusimama na kutembea tena kwa kutumia fimbo.
Susan anamtaarifu Alvira kuwa Lupe atakuwa anaishi nao kwa muda wote wa matatizo yao jambo hilo linampa matumaini Alvira akiamini kuwa Lupe atakuwa msaaada mkubwa kwao ili kumfanya Gary afungwe gerezani. Huku akitaka kuwa eneo watakalomuweka Lupe liwe la siri.
Familia ya Del Valles inafika mahakamani kwa ajili ya kesi ya Gary,
Clara anamkuta Mara akiwa katika chumba cha mapumziko anaanza kupayuka na kuanza mabishano ambayo yanamkera Alvira ambapo anachukua jukumu la kumpiga vibao Clara kwa kumsema hovyo Mara.
Gary anawafuatilia Amanthe na Alvira na kugundua nyumba mpya wanayoishi Alvira anakuwa wa kwanza kumuona Gary akiwa nje ya nyumba yao hiyo mpya, kwa haraka anaita polisi kutokana na kukaidi oda ya maakama baaada ya kufunguliwa mashitaka na Alvira. Lakini wakati Alvira akifanya hivyo, Clara anakwenda kusachi kwa Gary na kukuta kifaa cha kurekodia.
Siku ya kusikilizwa kesi inafika ambapo wakili wa Gary anaeleza kuwa Alvira na Gary walikuwa na urafiki wa karibu sana huku akieleza kuwa shahidi muhimu na pekee atakayekuja kuthibitisha hilo ni binti yake Clara Davidi. Je, unafikiria Clara ataeleza nini mahakamani na atakuwa upande Gary ama Amanthe?
0755-625042 au fstpolea@yahoo.com.