THE LEGAL WIFE
STAR wa
kike wa kifilipino Angel Locsin (Monica) leo tunaendelea kuangalia historia ya
maisha yake baada ya kutambua tangu alipozaliwa hadi alivyoingia katika
uigizaji.
Pia
tumeona namna alivyokuwa akishirikiana na wazazi wake katika mambo ya mikataba
ya kazi huku akielekezwa namna salama kwa kufanya kazi hiyo ya uigizaji wake.
Ni
mtoto anayetokea familia ya kisultani amezaliwa April 23 mwaka 1985 katika mji
wa Bulacan nchini Ufilipino ni mtu maarufu sana nchini humo kutokana na uwezo
wake mkubwa wa kuigiza kwa ufanisi mkubwa.
Leo
tunaangazia uhusiano wake wa kimapenzi ukoje? Muigizaji huyu anayetamba kwa
jina la Monica kupitia tamthilia ya ‘The Legal Wife’ amewahi kukiri kwamba
anazidi kumpenda aliyewahi kuwa mpenzi wake Luis Manzano.
Mwanaume huyo
aliwahi kuwa na uhusiano naye miaka minne iliyopita lakini ameibuka na
kutangaza kwamba anaendelea kumpenda na anataka kuendelea kuwa naye.
"Siwezi
kuelezea namna gani nahisia kwa sasa lakini ninachojua ni kwamba nampenda na
ninataka kuwa naye,’’ alieleza katika mahojiano hayo na kituo kimoja wapo cha
runinga nchini humo.
Alipohojiwa
kama anataka kurudiana na mwanaume huyo awali katika mahojiano yake huko Bandila alisema
kwamba anaamini anampenda na anataka kuwa naye kwa kuwa hajampata kama huyo
mwanaume kwa muda wote wa miaka minne aliyoachana naye.
Kwa mujibu wa ABS-CBN, Monica alitoa la moyoni hilo alipokuwa katika
mahojiano na waandishi wa habari wakati walipokuwa wakitangaza ujio mpya wa
tamthilia ya ‘The Legal Wife’.
"Tuliachana
miaka minne iliyopita bila kuwasiliana lakini kwa sasa tumeanza kuwasiliana na
kuweka mambo sawa natumaini tutarudiana na kuwa pamoja kama zamani,’’ alieleza
huku akiweka wazi alikuwa akiumia kila walipokuwa wakikutana na mwanaume huyo
Ingawa alikuwa
akiumia lakini siku moja walipokutana katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa
sababu ya uigizaji waliamua kuvunja ukimya wao na kuzungumzia maisha yao ya
kimapenzi huku wakikubali kusahau yaliyopita ili waanze upya.
Check gazeti la Bingwa la leo