Harusi

BW. LUITFRID SINGUMLANJI NA BI. LUCIANA CHELELE
 

NOVEMBER 10/11/2012 NDOA ILIFUNGWA
 
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakisubiri kuanza kwa misa ya ndoa yao muda mfupi kabla hawajaunganishwa na kuwa mwili mmoja ambapo Bwana Luitfried Singumlanji na Bi. Luciana Chelele watakuwa mume na mke maisha yote labda kifo ndiyo kiwatengenishe. lakini watakuwa pamoja katika shida na laha popote pale, hakutakuwa na ugonvi wala ubondia kati yao pia mashemeji tunapomtembelea hatotunyima wali kwa njuju ahaaaaa!!! blog ya tamthilia inawatakia mafanikio mema katika maisha yao.
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa wameshika kwa makini vikombe maalum vilivyohifadhia mkate na divai tayari wakivielekeza altareni kwa ajili ya kuanza kwa ibada ya misa yao ya ndoa iliyofanyika Novemba 10, mwaka jana katika kanisa la mtakatifu, Andrea Ifakara.
Bi. Luciana Chelele na Luitfried Singumlanji wakisogelea altare tayari kabisa kwa zoezi la kuwaunganisha kuwa mwili mmoja na kuachana na majina yao na kuitwa mume na mke aliloliunganisha Mungu binadamu hawezi kulitengua.
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa katika nyuso za furaha pamoja na watoto ndugu na marafiki wa karibu kutoka pande mbili, wakiwa katika ufukwe wa kivuko cha Kilombero, muda mfupi baada ya ndoa yao iliyofungwa katika kanisa kuu la mtakatifu Andrea Ifakara Novemba 10 mwaka jana.
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa katika nyuso za furaha pamoja na wapambe wao katika hafla iliyofanyika katika Ifakara na kushuhudiwa na ndugu, jamaa na marafiki toka pande mbalimbali za mikoa pamoja na nchi za nje.
Safi, hapa sasa shemeji yetu ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi, Mlabani Ifakara ndiyo kapata mume sasa na kaka yetu ambaye naye ni Afisa Maendeleo Jamii anayefanya kazi na shirika la Plan International Tanzania tawi la Ifakara naye ndiyo kapata mke hapa wanapofurahia wameshafunga ndoa katika kanisa kuu la mtakatifu Andrew. Na hapa walipo ni katika kivuko cha Kilombero wakipata upepo mzuri na nyuso zao zinaonyesha furaha bashasha.

====================================================
 
MFANYAKAZI  wa Idara ya Matangazo katika kampuni inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizeni na Mwanaspiti, Mwananchi Communications ltd (MCL), Desmond Amlina hivi karibuni amefunga ndoa na Janepher Mkumbo, Songea mkoani Ruvuma.
              Desmund alikuwa Captein wa timu ya wasiooa lakini sasa ameamua kuhama timu hiyo kaona haina manufaa kwake maana wanaulizana sana tupo wangapi? kaamua kuamia kwenye timu ya nipo na huyu tu, tehe tehe teheeeee!! hongera Desmund.
Janepher Mkumboa akiwa saloni maeneo katika maandalizi ya kuelekea katika
sherehe yake ya kuagwa iliyofanyika Sinza jijini Dar es saslaam akiwa na mpambe wake anaitwa Hadija
Eheee! We Fredrick unamuona wife to be anavyoyarudi
kumbe anaweza kucheza ahaa!!! nimepata mke
Du! sijui Desmund ananiona, sijui anafurahia ninavyocheza eti Hadija? Anakuona
Karibuni mvinyo wanandugu, wapendwa wangu leo nawaaga
 nami hivi karibuni nitakuwa kwangu jina litabadilika kidogo nitaiwtwa Mrs. Desmund, mtanitaka
Mrs. Amlima hapa alikuwa mtarajiwa akiwa na mpambe wake, Bi. Hadija
 wakati wa sherehe ya kumuaga iliyofanyika jijini Dar es salaam maeneo ya Sinza

Dada na Kaka wanafuatilia kwa makini kabisa yanayotokea ukumbini hapa
hii ni send off jamani

'Nimekubamba ole wako ungejificha mbali nisingekutafuta' Janepher Mkumbo
 akiwa amefanikiwa kumpata mumewe lakini kipindi hicho alikuwa mtarajiwa wake. 
'Nishamuona kinachofuata kujisosomola karibuni wote ata mnaoniangalia kuitia blog hii
'Mke wangu natarajia zaidi ya hivi.......' 'We bado mi siyo mkeo ata ndoa bado unaniita mke.. sitaki'

Sasa mnaotuona mbele yenu ndiyo watarajiwa tukiwa na wapambe wetu,
 tunawakaribisha sana katika harusi yetu tutakayoifungia Songea
Hawa ni wanakamati wetu, walifanya kazi kubwa sana zaidi hata
ya wapiga kampeni wa Obama
Waangalie vizuri kwa hapa, hawana kinyongo ukiwahitaji katika sherehe yako
 wasiliana na
Desmund Amlima
'Siku ya Ndoa tunaelekea Kanisani'
Jamani tuimbe badi mwanetu kapendeza... aya shangazi anzisha ule wimbo wa kilugha..
Tumeshafika katika Kanisa katoriki la Bikira Maria Mjimwema, Songea
siyo Kigamboni wala Kigoma... wala siyo Moshi haoa ni Songea.
Desmund Amlima na Janepher Mkumbo wakiwa wamesimama imara kanisani
 wakimsikiliza Padre anayeongoza misa ambaye hayupo pichani
Waumini waliohudhuria siku ya harusihiyo iliyofanyika katika
Kanisa la Bikira Maria Mjimwema, Songea
Padri Finehas Amlima akaanza kutufungisha ndoa hapa ilifika wakati wa Desmund kuulizwa akaanza kujieleza Mimi Desmund Amlima nimekubali kwa moyo wangu kumuoa Janepher Mkumbo kwa...

Mambo yanaendelea, Pokea Pete hii uwe mke wangu wa maisha,
 tuvumiliane kwenye shida na laha, Mungu nisaidie

Nawe pokea pete hii uwe mume wangu wa ndoa, katika shida na laha
 nami sitakuacha maishani mwangu hadi kifo, Mungu nisaidie
Eheee! Wakaunganishwa kuwa mwili mmoja, Padri Finehas akiwaunganisha
 Desmund na Janepher  kama ishara ya mwili mmoja
Ninyi sasa mmnakuwa mwili mmoja sema haya,
 ' Mimi Desmund Amlima nimekubali kumuoa Janepher kuwa mke wangu
 katika shida na laha hadi kifo...
Jamani mbona hampigi vigeregere... mi nishamaliza hapa
 
Sasa mu mwili mmoja nendeni mkaijaze dunia,
 alilounganisha Mungu binadamu hawezi kutenganisha...Amina

Nawapa msalaba huu umaanishe ishara na uzidishe imani ya ulinzi
katika ndoa yenu aaminie ...

Bwana Desmund Amlima na Amani iwe nanyi mshakuwa mke na mume kwa Bwana
Tushakuwa mke na mume. Kutoka nje ya ndoa dhambi kwa Mungu
Ndoa teyari sasa ushahidi, Desmund Amlima akitia sahii katika
cheti chake cha ndoa huku mkewe kulia na padri aliyefungisha ndoa yao
 akiwa kushoto wakimuangalia kwa ukaribu. 
'Zamu yangu sasa' Bi Janepher akitia sahini katika cheti cha ndoa yao
Shahidi, somebody Kapinga naye alitia sahini huku Mrs Kapinga akimshuhudia
Eheee!! kumbe Mrs. Kapinga naye ndiye msimamizi wa Bi Janepher
safi sana mbwana na bibi...ahaaaaa!!!
Padri, Finehas akamalizia baada ya kuhakiki kama sahii
 za wanandoa hao ni sahii halisi naye alitia ya kwake ilikukamilisha uthibitisho
Ahaaaa!! Siamini .... ata mi siamini... ndiyo mmeshafunga ndoa sasa
 mkawe mke na mume mwema mambo ya panching beg hayana nafasi tehetehetehe!!!
Baada ya ndoa usiku wake tukaenda kujipongeza maana kuoa na kuolewa
 si kitu kidogo kinapaswa kupongezwa
Safi sanaaa Desmund na Janepher kuachana na kambi ya Ukapela safi mwanetu

Nasi tupo pamoja nanyi mkipatwa na jambo lolote jema baya mkiona linapaswa
kutushirikika tushirikisheni tutawasaidia kulitatua, Hongereni sana wanetu mkaishi salama.
Wenyewe tukaingia kufunga kazi, Ahaaa asikwambie mtu kuoa laha mh!!!! ata kuolewa laha Janepher si nimeolewa nafurahia ndoa yangu na Desmund Ahaaaa! safiii safi sanannnaa
Tulikuwa kama wafalme, nilijiona kama mswati ahaaa siyomswati kama chifu wa songea na mke wangu kama malkia wa.... ahaaaaaa!!!
Wamependeza sana au siyo kama haufurahii we mchawi...
Hapa kuna watu wawili mmoja ni Padri mwingine ni MC sasa kazi kwako
Padri yupo wapi na Mc YU WAPI?
Mimi naitwa ..... nipeni mji ili niwatajie....huko siendi nipe mji mwingine..
aha! mmechelewa basi siwatajii
 Yote kwa yote Ndoa ilifana sana msiooa na kuolewa muombeni Mungu awapatie mke na mume wema.

No comments:

Post a Comment

Comment