IVORY Coast imetinga nusu fainali ya
michuano ya AFCON kwa kuibanjua vinara wa Afrika katika soka Algeria kwa magoli
3-1 katika mchezo uliochezwa jana usiku.
Mabao ya Ivory yalifungwa na mchezaji
mpya wa Manchester City, Wilfred Bony ambaye alifunga mabao mawili yote kwa
kichwa huku Gervinho akifunga bao moja kirahisi dakika za mwisho wa mchezo.
Bao pekee la Algeria lilifungwa na
Hilal Soudani kwenye kipindi cha pili.
Ivory Coast watapambana na Congo DRC
katika mchezo wa nusu fainali huku Ghana wakicheza nusu fainali yao na wenyeji
wa michuano hii Equatorial Guinea.
No comments:
Post a Comment
Comment