Wasanii Wetu

IKIWA siku moja imepita tangu tuukaribishe mwaka 2013 na siku kadhaa baada ya Jopo la madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutoa ripoti mpya kuwa mwigizaji wa filamu nchini, Juma Kilowoko maarufu kwa jina ma Sajuki kuwa anasumbuliwa na kansa ya ngozi, msanii huyo leo amefarki dunia akiwa katika hospitalini hapo.
       Madaktari hao waligundua ugonjwa huo wa kana ya ngozi mwishoni mwa wiki baada ya kufanya uchunguzi wa kina ambapo waliukamilisha Desemba 29 mwaka jana na kuugundua ugonjwa huo.
         Hivi karibuni msanii huyo alianguka jukwani wakati akisalimia mashabiki wake waliofika katika tamasha aliloliandaa kwa lengo la kuchangisha fedha za kumuwezesha kupata matibabu, tamasha lililofanyika jijini Arusha lakini ata hivyo hali hiyo ililazimika kurudishwa jijini Dar es salaam na kulazwa katika hospitali ya Amana kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.
        Sajuki amefariki wakati harakati zikifanyika ili kumpeleka India kwa matibabu zaidi ambapo kwa inadaiwa kuwa Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff) ilishaandika barua kwa ajili ya kuipeleka Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete ikieleza tatizo ambalo msanii huyo analo ambapo barua hiyo ililenga kuomba msaada kwa Ikulu kuweza kumpeleka msanii huyo India kwa matibabu zaidi.
      Lakini kabla hilo halijakamilika Mungu amemchukua Pumzika kwa Amani 'Jembe' Sajuki, Pole sana Wastara blog hii ya 'tamthilia.blogspot.com' inawapa pole Wastara na familia zote mbili ya Sajuki na Wastara pamoja na ndugu na jamaa pia kwetu wote tulipenda kazi zake na kumsapoti hadi mwisho wa uhai wake hapa Duniani yeye ametangulia sisi tupo nyuma yake......Amen.




No comments:

Post a Comment

Comment