Tuesday, July 1, 2014

BE CAREFUL WITH MY HEART - RICHARD WIVU TUPU KWA MAYA





TAMTHILIA ya ‘Be Careful with my Heart itaendelea leo usiku kwa kumuonyesha Rafi na Charlie, na baada ya kuvishana pete wanaonekana kutokuendelea kuishi katika nyumba ya Lim.
     Lakini wakiwa wanajiandaa kuondoka katika nyumba hiyo, Maya, na watu wengine katika nyumba hiyo wanapanga kumfanyia sherehe ya kumuaga Rafi na Charlie.
     Katika sherehe hiyo, wakapanga wawe wawili wawili ili kuvutia tafrija hiyo lakini kila mmoja anapata wa kucheza naye isipokuwa Maya anajikuta akiwa peke yake.
     Maya baada ya kujiona yupo peke yake anasema hajali kuimba akiwa peke yake lakini licha ya hivyo wimbo wa Maya unatakiwa uimbwe na watu wawili kutokana na sauti ya kike na ya kiume.
        Anaanza kuimba kwa hisia kubwa, inawagusa watu wote akiwemo Richard. Lakini licha ya yote anapatwa na mshangao, baada ya kusikia sauti ya kiume ikiimba tena ni ya Richard, lakini sauti hiyo ilikuwa inaimba kwa kutokwenda na biti jambo lililozua kicheko zaidi.
       Wakiwa wanaelekea uwanja wa ndege, Rafi anampigia Richard anamtaka amwahidi kama atampigia simu kama atampata msichana atakayempenda tena kama ilivyokuwa kwa marehemu mke wake.
      Richard anakubaliana na hilo huku akitabasam mwenyewe. Baada ya muda, Kutengana kwa Cristina Rose (kute) na mtoto wake kunazua matatizo makubwa tofauti na alivyokuwa akifikiria awali.
      Hali hiyo inamfanya azungumze na viongozi wake huku akiwaeleza kwamba anapenda kufanyakazi katika meli aamini kama mtoto wake anaweza kukua bila kuwa karibu yake.
       Maya anapanga tarehe ya kukutana na Simon lakini anapata simu kutoka kwa Richard akimuomba amsaidie kumtafutia Abby rafiki wa kucheza naye lakini Maya anapozungumza na Abby anamweleza kwamba ingawa hakuna michezo ya kuangushana lakini urafiki wao unaendelea kama kawaida.
       Lakini licha ya hayo anamwahidi Abby kwamba atamtafutia rafiki mara tu atakaporejea. Mara baada ya Maya kurudi nyumbani, Richard anajifanya kama hajali huku akionekana mwenye hasira.
     Maya anahofia hali ya upole wa bosi wake, anamuomba msamaha huku akimweleza kwamba hakutaka amsumbue kwa kuwa anakazi lakini ukweli ni kwamba aanacheza ‘gemu’ la karata katika kompyuta yake mpakato.
     Maya anamweleza Miss Fe kuhusu ukimya wa Richard. Miss Fe anamwakikishi kwamba Richard hawezi kuigiza vile kama amwofii Maya na maisha yake ya baadae. Maya anaonekana kufurahia jambo hilo kusikia Richard anamjali katika hilo.
     Siku ya pili asubuhi, Richard anasikia mazungumzo ya Maya na Simon. Simon anataka kuwachukua Cristina Rose na Maya hadi stendi. Maya anakubali lakini Richard anajitolea kuwachukua Maya na Cristina Rose hadi stendi huku akionekana mnyenyekevu kwao.


No comments:

Post a Comment

Comment