Monday, February 11, 2013

BW. LUITFRID SINGUMLANJI NA BI. LUCIANA CHELELE

NOVEMBER 10/11/2012 NDOA ILIFUNGWA
  
 Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakisubiri kuanza kwa misa ya ndoa yao muda mfupi kabla hawajaunganishwa na kuwa mwili mmoja ambapo Bwana Luitfried Singumlanji na Bi. Luciana Chelele watakuwa mume na mke maisha yote labda kifo ndiyo kiwatengenishe. lakini watakuwa pamoja katika shida na laha popote pale, hakutakuwa na ugonvi wala ubondia kati yao pia mashemeji tunapomtembelea hatotunyima wali kwa njuju ahaaaaa!!! blog ya tamthilia inawatakia mafanikio mema katika maisha yao.
 
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa wameshika kwa makini vikombe maalum vilivyohifadhia mkate na divai tayari wakivielekeza altareni kwa ajili ya kuanza kwa ibada ya misa yao ya ndoa iliyofanyika Novemba 10, mwaka jana katika kanisa la mtakatifu, Andrea Ifakara. 
 
Bi. Luciana Chelele na Luitfried Singumlanji wakisogelea altare tayari kabisa kwa zoezi la kuwaunganisha kuwa mwili mmoja na kuachana na majina yao na kuitwa mume na mke aliloliunganisha Mungu binadamu hawezi kulitengua.
 
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa katika nyuso za furaha pamoja na watoto ndugu na marafiki wa karibu kutoka pande mbili, wakiwa katika ufukwe wa kivuko cha Kilombero, muda mfupi baada ya ndoa yao iliyofungwa katika kanisa kuu la mtakatifu Andrea Ifakara Novemba 10 mwaka jana.
 
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa katika nyuso za furaha pamoja na wapambe wao katika hafla iliyofanyika katika Ifakara na kushuhudiwa na ndugu, jamaa na marafiki toka pande mbalimbali za mikoa pamoja na nchi za nje.
 
Safi, hapa sasa shemeji yetu ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi, Mlabani Ifakara ndiyo kapata mume sasa na kaka yetu ambaye naye ni Afisa Maendeleo Jamii anayefanya kazi na shirika la Plan International Tanzania tawi la Ifakara naye ndiyo kapata mke hapa wanapofurahia wameshafunga ndoa katika kanisa kuu la mtakatifu Andrew. Na hapa walipo ni katika kivuko cha Kilombero wakipata upepo mzuri na nyuso zao zinaonyesha furaha bashasha.