USWISI ikiongozwa na Xherdan Shaqiri katika ushambuliaji imeshindwa kutamba mbele ya Argentina iliyoongozwa na Lionel Mess,ambayo imeifunga Uswisi kwa goli 1.
Uswisi ilikuwa na ukuta mgumu na mpira ulioeleweka lakini safu ya umaliiaji ilikuwa butu baada ya kukosa magoli mengi. Hata hivyo kipa alikuwa na uwezo mkubwa wa kuokoa michomo kutoka kwa washambuliaji wa Argentina akiwemo Maria na Messi.
Wakati huo huo, Marekani nayo imetupwa nje ya mashindano hayo na Ubelgiji, baada ya kufungwa magoli 2-1. Marekani walikuwa na bahati lakini hawakuitumia vizuri kwani walipata nafasi nyigi za wazi za kufunga lakini walishindwa kufanya hivyo.
Hatua inayofuatwa itaendelea Ijumaa baada ya kuwa na mapumziko ya siku mbili kwa timu zilizofuzu atua inayofuata kujipanga kwa mechi zao.
Hatua inayofuatwa itaendelea Ijumaa baada ya kuwa na mapumziko ya siku mbili kwa timu zilizofuzu atua inayofuata kujipanga kwa mechi zao.
No comments:
Post a Comment
Comment