Thursday, February 12, 2015

ISABELA MKALI WA KUIMBA NA KUCHEZA JUKWAANI

 Isabel Novella, mwimbaji kutoka Msumbiji, roots, traditional
Isabel Novella amezaliwa Maputo amezawadiwa sauti nyororo ya kuimbia, pia ni mwandishi wa nyimbo zakeawapo jukwaani hujawa na tabasamu pana lenye bashasha ni msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuimba na kucheza.
 Culture musical club
Culture musical club

ALI KIBA AFANYA MAKUBWA DAY ONE SAUTI ZA BUSARA

MSANII mashuhuri nchini Tanzania Ali Kiba leo usiku amefanya makubwa katika ukumbi wa Ngome kongwe kwa kuangusha bonge la shoo viziwani Zanzibar huku akishangiliwa wakati wote na mashabiki wake waliojaa uwanjani hapo.
       Onyesho lake hilo lilianza majira ya saa sita kasorobo akaendelea hadi majira ya saa saba na dakika zake ambapo umati ulilipuka kwa shangwe kila wakati alipoimba nyimbo zake tofauti.
       Onyesho hilo pia alimshirikisha mdogo wake Abdu Kiba naye alionyesha makeke mengi kwa kukatika kiuno huku wakicheza na kuimba kwa madaha ya namna yake.
       Licha ya kutokea hitirafu ndogo za mic lakini mashabiki waliimba na kushangilia na wasanii hao mwanzo hadi mwisho wa onyesho lao alilomaliza kwa kuimba wimbo wa Mwana Dar es Salaam.


 
 Ali Kiba akiwa na mdogo wake Abdul Kiba wakishambulia jukwaa

 Ali Kiba akiwa na mdogo wake Abdul Kiba wakishambulia jukwaa
 Baadhi ya mashabiki wakifuatilia kwa makini shoo ya Ali Kiba
Ali Kiba akiwa na mdogo wake Abdul Kiba wakishambulia jukwaa

UFUNGUZI WA SAUTI ZA BUSARA 2015 VISIWANI ZANZIBAR

TAMASHA la Kimataifa la Muziki la Sauti za Busara 2015, limefunguliwa huku wasanii mbalimbali wakionyesha uwezo wao jukwaani ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe Visiwani Zanzibar.

Wakati tamasha hilo likiendelea kumbi mbalimbali katika eneo hili zilikuwa zikiendelea na shughuli nyingine za burudani ikiwemo uonyeshwaji wa filamu mbalimbali.
   
Tamasha la Sauti za Busara kila mwaka katika ufunguzi wake huambatana na paredi huku umati wa watu wakijumuika pamoja na kusherehekea kwa amani kwa kuanza na maandamano hadi Ngome Kongwe. Leo ilianzia Magereza Miembeni hadi Ngome Kongwe.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri kwenye ufunguzi huo.
Parade on route photo Peter BennettIMG_6872
at Sauti za Busara 2015 (photo: Masoud Khamis)
IMG_7072
IMG_9129
IMG_9124

IMG_7064
 Ratiba ya yatakayojiri kwenye Tamasha la Sauti za Busara iko hapa chini.
IMG_9331
Shamra shamra za ufunguzi wa tamasha la Sauti za Busara 2015.