MSANII mashuhuri nchini Tanzania Ali Kiba leo usiku amefanya makubwa katika ukumbi wa Ngome kongwe kwa kuangusha bonge la shoo viziwani Zanzibar huku akishangiliwa wakati wote na mashabiki wake waliojaa uwanjani hapo.
Onyesho lake hilo lilianza majira ya saa sita kasorobo akaendelea hadi majira ya saa saba na dakika zake ambapo umati ulilipuka kwa shangwe kila wakati alipoimba nyimbo zake tofauti.
Onyesho hilo pia alimshirikisha mdogo wake Abdu Kiba naye alionyesha makeke mengi kwa kukatika kiuno huku wakicheza na kuimba kwa madaha ya namna yake.
Licha ya kutokea hitirafu ndogo za mic lakini mashabiki waliimba na kushangilia na wasanii hao mwanzo hadi mwisho wa onyesho lao alilomaliza kwa kuimba wimbo wa Mwana Dar es Salaam.
Ali Kiba akiwa na mdogo wake Abdul Kiba wakishambulia jukwaa
Ali Kiba akiwa na mdogo wake Abdul Kiba wakishambulia jukwaa
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia kwa makini shoo ya Ali Kiba
Ali Kiba akiwa na mdogo wake Abdul Kiba wakishambulia jukwaa
No comments:
Post a Comment
Comment