TAMASHA la Kimataifa la Muziki la Sauti za Busara 2015, limefunguliwa huku wasanii mbalimbali wakionyesha uwezo wao jukwaani ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe Visiwani Zanzibar.
Wakati tamasha hilo likiendelea kumbi mbalimbali katika eneo hili zilikuwa zikiendelea na shughuli nyingine za burudani ikiwemo uonyeshwaji wa filamu mbalimbali.
Tamasha la Sauti za Busara kila mwaka katika ufunguzi wake huambatana na paredi huku umati wa watu wakijumuika pamoja na kusherehekea kwa amani kwa kuanza na maandamano hadi Ngome Kongwe. Leo ilianzia Magereza Miembeni hadi Ngome Kongwe.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio yaliyojiri kwenye ufunguzi huo.
Ratiba ya yatakayojiri kwenye Tamasha la Sauti za Busara iko hapa chini.
Shamra shamra za ufunguzi wa tamasha la Sauti za Busara 2015.
No comments:
Post a Comment
Comment