TAMASHA la ‘Zanzibar
Fashion Gala’ limefanyika Visiwani Zanzibar kwa mafanikio makubwa baada
ya kukubaliwa na wazee wa Visiwani humo kwamba fashioni siyo uhuni kama inavyodhaniwa na wengi.
Mratibu wa
Tamasha hilo, Titi alisema ilikuwa kazi kuwafanahamisha wazee kuhusiana na
maonyesho hayo ya urembo, hadi walipowaelezea faida ya urembo kwa msichana wa Zanzibar kwamba anajitengenezea ajira
na mambo mengine mengi.
Titi alisema dhunini la onyesho hilo lililofanyika katika fukwe za bahari ni
kuboresha fani ya ubunifu wa mavazi visiwani Zanzibar pamoja na kuvionyesha na kuvikuza vipaji vya
wasichana wa Zanzibar .
Mengine ni kutoa
ajira kwa wasichana warembo, kuwafundisha nidhamu, kuwajengea kujiamini na
wajielewe ili wasijihusishe na matendo mabaya yatakayowaharibia maisha yako.
No comments:
Post a Comment
Comment