MSANII kutoka Nigeria Davido ameshinda tuzo ya ‘Best International Act. Afrika’huku swahiba wake Diamond akikosa tuzo hiyo lakini amejipatia umaarufu mkubwa kutoka kwa mashabiki wake kote duniani baada ya kufika hatua ya juu na kuweka historia kwa kuwa mwakilishi pekee wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2014.
Davido akiwa na tuzo yake
Wasanii walioshindania
tuzo hiyo ni Diamond Platnumz (Tanzania), Davido (Nigeria), Mafikizolo (Afrika
Kusini), Sarkodie (Ghana),
Tiwa Savage (Nigeria) na Toofan
wa (Togo).
Baada
ya tuzo hizo, Davido aliandika kwenye ukurasa wake wa ‘Instagram’ alishukuru
mashabiki wake na kuelezea furaha yake kwamba wamepata tuzo hiyo.
Diamond kupitia ukurasa wake wa ‘Instagram’
alisema nanukuu; “Kupata fursa ya ‘kushare treatment', ‘kunetwork’ na kubadili ‘ideas’
na wasanii ambao ulikuwa ukiwaona tangu mtoto, unakua na tangu unaanza muziki
haujui utoke vipi... kiukweli ni jambo ambalo linatia moyo na nguvu sana ili
uzidi kupambana zaidi, kesho na kesho kutwa, tasnia yetu nasi ifike kwenye
kilele... ‘Das me and my Boy Nelly at the @betawards red carpet’... Wenyewe wa
uswazi tunamuitaga "Nelly I love you" Mzee wa plasta’’ ulieleza
ujumbe huo ulioambatana na picha ya Diamond akisalimiana na msanii wa Marekani
Nelly.
Diamond akiwa na Nelly
Hata hivyo utoaji wa tuzo hizo umewakera watanzania wengi kutokana na kutokuwa na
mpangilio mzuri huku tuzo zikitolewa tofauti na utaratibu uliozoeleka kwenye
tuzo mbalimbali ikiwemo MTV base.
Hata hivyo baadhi ya watu wameponda utaratibu wa tuzo ulivyokuwa ukitolewa kwa baadhi ya wasanii kuonekana jukwaa kuu huku wengine wakiishia backstage na wengine wakionekana kushika tuzo zao.
No comments:
Post a Comment
Comment