BAADA ya kushangaza wengi alipohudhuria katika sherehe ya
Zari All White Party iliyoandaliwa na msanii Abdul Nasib ‘Diamond’ anayedaiwa
kutoelewana naye, prodyuza Raheem Rummy ‘Bob junior’ ameendelea kushangaza
wengi kwa madai kwamba wapo mbioni kurekodi wimbo wa pamoja na msanii huyo.
Prodyuza huyo aliweka wazi mipango yake hiyo huku akidai
tayari ameishanunua baadhi ya vifaa vipya kwa ajili ya kuimarisha studio yake
iwe katika ubora wa kimataifa kama studio nyingine zinazoongoza kwa ubora
duniani.
“Hiyo ni zaidi ya ‘surprise’, kwa ubora wa vyombo vyangu
ninaimani ‘beat’ itakayotoka hapo itakuwa kwenye kiwango cha hali ya juu na
kazi yetu itakuwa nzuri sana,” alimaliza.
Source Mtanzania
No comments:
Post a Comment
Comment