Monday, February 18, 2013

ASKARI WANYAMAPORI WAUA SIMBA ALIYEKULA MBUZI 47

 MOROGORO


Wakazi wa kijiji cha Bagilo kata ya Kinole halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakiwamwangalia simba aliyeuawa na askari wa wanyamapori wa halmashauri hiyo baada ya simba huyo kukamata na kuua mbuzi 47 katika vijiji vitano tofauti vya tarafa ya Mkuyuni mkoani hapa jana. 
Mwanablog Juma Mtanda akimkagua Simba huyo mara baada ya kufikishwaa katika ofisi za Maliasili mkoani Morogoro muda mfupi kabla ya kuchunwa ngozi.
Afisa wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Iddi Ndabagenga akimkagua simba huyo.
Askari wa wanyamapori wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro Abdallah Mayingi kushoto na Jontas Sume kulia ndiyo waliohusika katika zoezi la kumua simba huyo.
Hapa zoezi la kumchuna ngozi likiufanyika katika ofisi za maliasili Morogoro

Sunday, February 17, 2013

KIPINDI CHA DK RAHABU NA VIDONDA VYA TUMBO CHA STAR TV KINAVYOANDALIWA

 
 
 
HAPA ni ubungo plaza ambapo ndipo cliniki ya Rahabu Urlcers Clinic ilipo ambapo wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanapatiwa tiba kupitia dawa ya Fiterawa na kupona ugonjwa huo kabisa. Dr. Rahabu Rubago anapatikana kwa namba 0784-338513, 0754-411119
 
Hapa nakuonyesha namna ambavyo kipindi cha Dk Rahabu na Vidonda vya tumbo kinavyoandaliwa hadi kurushwa kupitia televisioni ya Star tv
Bi shosti, mgeni siku hiyo mtized kutoka Uingereza, ambaye ni mwanablogerTina
Huyu alikuwa mtangazaji wa kipindi hicho pia ni mtangazaji wa kweli anafanya kazi na Chanel 10
Huyu alikuwa mpiga picha za mnato sijui kiswahili ni sawa zile za kutembea zile
Mitambo inaandaliwa hapa mapouda yanapakwa taa zinawashwa kila kitu kinawekwa sawa
Simu zinazimwa ama kutolewa sauti ili zisiingiliane na kurekodi
 
 
Ebana angalia hilo mic lako lisije likadondoka likatuchafua meen ahaaaaa!!
Liwachafue wapi subirini niwatengeneze muuze sura hizo, wekeni pozi niwafotoe
Ebana mi nafikiri tupo sawa tunaweza kuanza maana tushajiandaa vya kutosha
  Haya stand by, happy sirudii ahaaa!! Action
 Mahojiano yanakwenda maswali na majibu usikose kutazama Jumamosi hii ni hatari balaa kipindi kipo moto mbayaaa!!! 
 Kwa hiyo Uingereza alivyokuja watu wamepokeaje huko... 
 Ahaaa stop, kuna kitu hakipo sawa hapo dada huonekani kama upo sawa dokta naye kule sasa tunarudia Happy...Action
 
 
 Yap! Hapa mpo sawa embu ngojeni niwapige na picha za steel
 Wekeni pozi basi majamen keeee!! 
 Ahaaaaa tumemaliza kushuti kipindi cha wiki Jumamosi ijayo

 Kazi ya kurekodi huwa inakuwa ngumu jamani nashukuru nimemaliza salama tuna kila sababu ya kujipongeza kulia ndiye muongozaji mtangazaji Boniphace na kulia ni mwanabloger anayefanyia shughuli zake nchini Uingereza licha ya kuwa mtangazaji wa kituo cha tv kimoja wapo nchini humo ni mtanzania anayependa zaidia mambo ya (Current Affairs)
 
 
 Unamuona hapa alirekodi kipindi akiwa Arusha
 Kazi kubwa hadi unapokiona kikienda hewani yote ni Mapenzi ya Mungu
Kazi imeisha ndiyo tunamuona Dk Rahabu Rubago kupitia terevisioni ya Star tv siku ya Jumamosi saa 4 usiku
Si rahisi kama unavyofikiria ni kazi kubwa lakini Mungu anasaidia vinapendwa sana vipindi hivi vya Dk Rahabu na Vidonda vya Tumbo vinavyoonyeshwa kupitia televisioni ya Star tv.
 

Monday, February 11, 2013

BW. LUITFRID SINGUMLANJI NA BI. LUCIANA CHELELE

NOVEMBER 10/11/2012 NDOA ILIFUNGWA
  
 Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakisubiri kuanza kwa misa ya ndoa yao muda mfupi kabla hawajaunganishwa na kuwa mwili mmoja ambapo Bwana Luitfried Singumlanji na Bi. Luciana Chelele watakuwa mume na mke maisha yote labda kifo ndiyo kiwatengenishe. lakini watakuwa pamoja katika shida na laha popote pale, hakutakuwa na ugonvi wala ubondia kati yao pia mashemeji tunapomtembelea hatotunyima wali kwa njuju ahaaaaa!!! blog ya tamthilia inawatakia mafanikio mema katika maisha yao.
 
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa wameshika kwa makini vikombe maalum vilivyohifadhia mkate na divai tayari wakivielekeza altareni kwa ajili ya kuanza kwa ibada ya misa yao ya ndoa iliyofanyika Novemba 10, mwaka jana katika kanisa la mtakatifu, Andrea Ifakara. 
 
Bi. Luciana Chelele na Luitfried Singumlanji wakisogelea altare tayari kabisa kwa zoezi la kuwaunganisha kuwa mwili mmoja na kuachana na majina yao na kuitwa mume na mke aliloliunganisha Mungu binadamu hawezi kulitengua.
 
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa katika nyuso za furaha pamoja na watoto ndugu na marafiki wa karibu kutoka pande mbili, wakiwa katika ufukwe wa kivuko cha Kilombero, muda mfupi baada ya ndoa yao iliyofungwa katika kanisa kuu la mtakatifu Andrea Ifakara Novemba 10 mwaka jana.
 
Bi. Luciana Chelele na mumewe Luitfried Singumlanji wakiwa katika nyuso za furaha pamoja na wapambe wao katika hafla iliyofanyika katika Ifakara na kushuhudiwa na ndugu, jamaa na marafiki toka pande mbalimbali za mikoa pamoja na nchi za nje.
 
Safi, hapa sasa shemeji yetu ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi, Mlabani Ifakara ndiyo kapata mume sasa na kaka yetu ambaye naye ni Afisa Maendeleo Jamii anayefanya kazi na shirika la Plan International Tanzania tawi la Ifakara naye ndiyo kapata mke hapa wanapofurahia wameshafunga ndoa katika kanisa kuu la mtakatifu Andrew. Na hapa walipo ni katika kivuko cha Kilombero wakipata upepo mzuri na nyuso zao zinaonyesha furaha bashasha.