Monday, June 30, 2014
NAOMBA TUPIGE PICHA JAMANI
Ahaaaa! nimepiga picha na Shamsa Ford am Happy now star wa ukweee! alisema dada huyo aliyefahamika kwa jina la Lucy mara baada ya kuangaika kumsaka Shamsa Ford kwa lengo la kupiga naye picha alipompata roho yake ikawa kwatu, ahaaa safi sana katimiza ndoto zake za kupuiga picha na Shamsa Ford.
He! Jamani Zamaradi naomba tupige picha na wewe mimi Modo wa Zanzibar!
Kama mapacha wa familia tofauti
Ni picha tu Jamani tusitafutane
Friends Forever, nasi tulikuwepo mnatuonaje?
Du! Eti dada Mnigeria, anaitwa Mimi naye alitamani muda mrefu kupigapicha na J.Silk mtangazaji wa TBC kipindi Ulimwengu wa Filamu.
UREMBO ZANZIBAR SI UHUNI, WAZEE WANENA
TAMASHA la ‘Zanzibar
Fashion Gala’ limefanyika Visiwani Zanzibar kwa mafanikio makubwa baada
ya kukubaliwa na wazee wa Visiwani humo kwamba fashioni siyo uhuni kama inavyodhaniwa na wengi.
Mratibu wa
Tamasha hilo, Titi alisema ilikuwa kazi kuwafanahamisha wazee kuhusiana na
maonyesho hayo ya urembo, hadi walipowaelezea faida ya urembo kwa msichana wa Zanzibar kwamba anajitengenezea ajira
na mambo mengine mengi.
Titi alisema dhunini la onyesho hilo lililofanyika katika fukwe za bahari ni
kuboresha fani ya ubunifu wa mavazi visiwani Zanzibar pamoja na kuvionyesha na kuvikuza vipaji vya
wasichana wa Zanzibar .
Mengine ni kutoa
ajira kwa wasichana warembo, kuwafundisha nidhamu, kuwajengea kujiamini na
wajielewe ili wasijihusishe na matendo mabaya yatakayowaharibia maisha yako.

Monday, February 18, 2013
ASKARI WANYAMAPORI WAUA SIMBA ALIYEKULA MBUZI 47
MOROGORO
Wakazi wa kijiji
cha Bagilo kata ya Kinole halmashauri ya wilaya ya Morogoro wakiwamwangalia
simba aliyeuawa na askari wa wanyamapori wa halmashauri hiyo baada ya simba huyo
kukamata na kuua mbuzi 47 katika vijiji vitano tofauti vya tarafa ya Mkuyuni
mkoani hapa jana.
Mwanablog Juma Mtanda akimkagua Simba huyo mara
baada ya kufikishwaa katika ofisi za Maliasili mkoani Morogoro muda mfupi kabla
ya kuchunwa ngozi.
Afisa wanyamapori halmashauri ya wilaya ya Morogoro, Iddi
Ndabagenga akimkagua simba huyo.
Askari wa
wanyamapori wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro Abdallah Mayingi kushoto na
Jontas Sume kulia ndiyo waliohusika katika zoezi la kumua simba
huyo.
Hapa zoezi la
kumchuna ngozi likiufanyika katika ofisi za maliasili Morogoro
Sunday, February 17, 2013
KIPINDI CHA DK RAHABU NA VIDONDA VYA TUMBO CHA STAR TV KINAVYOANDALIWA
HAPA ni ubungo plaza ambapo ndipo cliniki ya Rahabu Urlcers Clinic ilipo ambapo wagonjwa wa vidonda vya tumbo wanapatiwa tiba kupitia dawa ya Fiterawa na kupona ugonjwa huo kabisa. Dr. Rahabu Rubago anapatikana kwa namba 0784-338513, 0754-411119
Hapa nakuonyesha namna ambavyo kipindi cha Dk Rahabu na Vidonda vya tumbo kinavyoandaliwa hadi kurushwa kupitia televisioni ya Star tv
Bi shosti, mgeni siku hiyo mtized kutoka Uingereza, ambaye ni mwanablogerTina
Huyu alikuwa mtangazaji wa kipindi hicho pia ni mtangazaji wa kweli anafanya kazi na Chanel 10
Huyu alikuwa mpiga picha za mnato sijui kiswahili ni sawa zile za kutembea zile
Mitambo inaandaliwa hapa mapouda yanapakwa taa zinawashwa kila kitu kinawekwa sawa
Simu zinazimwa ama kutolewa sauti ili zisiingiliane na kurekodi
Ebana angalia hilo mic lako lisije likadondoka likatuchafua meen ahaaaaa!!
Liwachafue wapi subirini niwatengeneze muuze sura hizo, wekeni pozi niwafotoe
Ebana mi nafikiri tupo sawa tunaweza kuanza maana tushajiandaa vya kutosha
Haya stand by, happy sirudii ahaaa!! Action
Mahojiano yanakwenda maswali na majibu usikose kutazama Jumamosi hii ni hatari balaa kipindi kipo moto mbayaaa!!!
Kwa hiyo Uingereza alivyokuja watu wamepokeaje huko...
Ahaaa stop, kuna kitu hakipo sawa hapo dada huonekani kama upo sawa dokta naye kule sasa tunarudia Happy...Action
Yap! Hapa mpo sawa embu ngojeni niwapige na picha za steel
Wekeni pozi basi majamen keeee!!
Ahaaaaa tumemaliza kushuti kipindi cha wiki Jumamosi ijayo
Kazi ya kurekodi huwa inakuwa ngumu jamani nashukuru nimemaliza salama tuna kila sababu ya kujipongeza kulia ndiye muongozaji mtangazaji Boniphace na kulia ni mwanabloger anayefanyia shughuli zake nchini Uingereza licha ya kuwa mtangazaji wa kituo cha tv kimoja wapo nchini humo ni mtanzania anayependa zaidia mambo ya (Current Affairs)
Unamuona hapa alirekodi kipindi akiwa Arusha
Kazi kubwa hadi unapokiona kikienda hewani yote ni Mapenzi ya Mungu
Kazi imeisha ndiyo tunamuona Dk Rahabu Rubago kupitia terevisioni ya Star tv siku ya Jumamosi saa 4 usiku
Si rahisi kama unavyofikiria ni kazi kubwa lakini Mungu anasaidia vinapendwa sana vipindi hivi vya Dk Rahabu na Vidonda vya Tumbo vinavyoonyeshwa kupitia televisioni ya Star tv.
Subscribe to:
Posts (Atom)






